HabariPilipili FmPilipili FM News

Mitambo 17 Ya Gari Moshi Yawasili Bandarini.

Serikali kupitia wizara ya uchukuzi imepokea mitambo 17 ya gari moshi katika bandari ya Mombasa itakayobeba mabogi ya mizigo na abira.

Katibu katika wizara ya uchukuzi nchini Paul Mwangi  amesema serikali  imeagiza mabogi  1,620 akisema  hadi kufikia saa hii tayari mabogi 763 yameingia nchini.

Mwangi amesema njia ya Reli haitafunga kazi za usafiri wa gari za mizigo ambazo zimeajiri wakenya wengi, akisema gari za kubeba mizigi zitakuwa na kazi zao kama kawaidi, kupeleka mizigo maeneo ya Kenya ambayo hayajafikiwa na njia ya reli.

Show More

Related Articles