HabariMilele FmSwahili

Mchezo wa ‘Blue Whale’ wapigwa marufuku na bodi ya filamu nchini

Bodi ya filamu nchini(KFCB) imepiga marufuku mchezo wa ‘Blue Whale’ ambao umesababisha kifo cha mtoto mmoja nchini kufikia sasa. Mwenyekiti wa KFCB Ezekiel Mutua anasema hatua hiyo imechukuliwa baada ya mtoto mmoja aliyekua nashiriki mchezo huo kufariki eneo la Kamukunji hapa Nairobi. Katika kikao na wanhabari,Mutua anasema serikali itafanya kila iwezalo kumaliza mchezo huo nchini. Mutua anasema KFCB imeiandikia mitandao ya Google na Twitter isiruhusu michezo hiyo akionya watakaokiuka sheria kwamba watakabiliwa vilivyo.

Show More

Related Articles