MichezoPilipili FmPilipili FM News

Utata Wa Uhamisho Wa Pogba.

JUZI kuliibuka stori kuwa Uhamisho wa Rekodi ya Dunia wa Dau la Pauni Milioni 89.3 wa Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United Mwezi Agosti Mwaka Jana unachunguzwa na FIFA.

Ingawa FIFA wamesisitiza kuwa huu si uchunguzi rasmi licha kutaka maelezo zaidi toka kwa Vilabu vilivyohusika.

Lakini hatua hiyo imeshangaza kwani FIFA hao hao ndio wanaobariki Uhamisho wa Wachezaji Kimataifa kupitia Mfumo wao wa International Transfer Matching System (ITMS) ambao huhitaji taarifa zaidi ya 20 zikiwemo aina ya Uhamisho, Mawakala wanaohusika, Ulipwaji wa Ada zote na namna zitakavyolipwa.

Baada ya hayo kutimizwa FIFA hutoa Kibali na hilo ndilo lililofanywa kwenye Uhamisho wa Pogba na hivyo ndivyo ambavyo Klabu ya Manchester United ilivyoijibu FIFA kwamba hawana cha ziada mbali yay ale yaliyokuwemo kwenye ITMS.

Man United ilipewa Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa, ITC International Transfer Certificate, mara baada ya kukamilisha taratibu zote za Uhamisho wa Pogba kupitia Mfumo wa ITMS.

Lipi limejiri mpaka sasa FIFA kutaka Taarifa zaidi?

Mpaka sasa haijulikani kwanini FIFA wameibua haya kwa wakati huu.

Lakini Wachambuzi wanahisi kuwa hilo limetokana na kuchapishwa kwa Kitabu huko Germany Wiki hii, kiitwacho The Football Leaks: The Dirty Business of Football, ambacho, miongoni mwa kulipua mengi nyuma ya pazia kuhusu Soka, pia kiligusia ada kubwa mno aliyolipwa Wakala wa Pogba, Mino Raiola, kiasi cha kudaiwa kuvunja Kanuni za FIFA za Uhamisho wa Wachezaji.

Show More

Related Articles