HabariPilipili FmPilipili FM News

Kilio Cha Wakuliwa Wa Taita Kwa Serikali.

Wakulima katika kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuwasaidia kuvuna maji yanayoshuka kutoka milimani, kila wakati mvua inaponyesha ili kuyatumia wakati wa ukame.

Wakulima hao wanailaumu wizara ya kilimo katika kaunti hiyo kwa kushindwa kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji hayo licha ya wao kuahidi kufanya hivyo.

wanasema iwapo serikali itatimiza ahadi hiyo watapata  fursa  ya kufanya kilimo nyunyizi wakati wa ukame, hali ambayo wanasema itasaidia kuimarisha usalama wa chakula eneo hilo.

Show More

Related Articles