HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Wajitokeza Kwenye Zoezi La Kusajiliwa Kama Makurutu.

Mamia ya vijana wamejitokeza katika zoezi la kusajili makurutu wapya wa polisi katika uwanja wa Mvita hapa mjini Mombasa.

Akiongea na wanahabari msimamizi wa zoezi hilo katika eneo la mvita, Augustine Mwamburi amesema kufikia sasa hakuna visa vyovyote vya ufisadi vilivyoripotiwa huku akisema vijana wengi waliojitokeza hawakufikia viwango hitajika kimasomo.

Wakati huo huo amesema idadi ndogo ya wanawake imejitokeza kwenye zoezi hilo la leo ikilinganishwa na wanaume.

Amesema hatua hiyo imechangiwa na pendekezo la idara hiyo la kuaka kusajili wanawake wawili pekee kutoka eneo hilo.

Zoezi hilo linafanywa nchi nzima ambapo idara ya polisi inanuia kuwateuwa makurutu wapya elfu 10 kujiunga na idara hiyo.

Show More

Related Articles