HabariMilele FmSwahili

Caroli omondi ajiondoa katika kinyanganyiro cha ubunge Suba

Muaniaji kiti cha ubunge eneo la Suba kwa tiketi ya chama cha ODM Caroli Omondi amejiondoa katika kinyanganyiro hicho. Omondi amesusia zoezi hilo linaloandaliwa leo akidai chama cha ODM kinampendelea mbunge wa sasa John Mbadi. Omondi pia amesema atatoa maelezo kamili kuhusu hatua atakayochukuwa baadaye leo. Zoezi hilo  pia limekumbwa na utata huku masomo yakiendelea baadhi ya shule zilizopaswa kutumika kama vituo vya kupiga kura. Mchujo huo unarejelewa katika vituo saba vya Koga, Miria god oloo, Oma, Kiembe, Mukuyu na Nyakiya

Show More

Related Articles