Milele FmSwahili

Mikakati ya kupunguza gharama ya maisha

Maafisa kutoka wizara ya fedha wanakutana na wanakamati za bunge la taifa kuhusu bajeti na fedha kuangazia baadhi ya mikakati ambayo itawasilishwa bungeni kwa mujadala kukabiliana na gharama ya juu ya maisha. Mkutano huo unatumiwa kuandaa bajeti ya ziada ambayo itaratibu mwongozo utakaotumiwa na serikali kupunguza bei ya bidhaa muhimu. Kamati ya fedha pia imekutana na waziri wa fedha Henry Rotich kuhusiana na masuala haya. Hata hivyo changamoto kuu ambayo inakabiliwa mchakato huu ni kukosekana idadi inayostahili ya wabunge bungeni.

 

Show More

Related Articles