HabariPilipili FmPilipili FM News

Joho Ailaumu Serikali Kuhusu Kivuko Cha Ferry.

Shughuli za usafiri katika kivuko cha Likoni zimetatizika mapema hii leo kufuatia kupanda kwa viwango vya maji hali iliyotatiza usafiri wa kivuko hicho kwa masaa kadhaa.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa halimashauri ya Kenya ferry Bakari Goa hali hio imeshuhudiwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku za hivi karibuni hali ambayo imefanya ferry kuvutwa na maji wakati inapoegeshwa kushukisha abiria.

Kwa upande wao  baadhi ya watumiaji wa kivuko hicho wameulaumu usimamizi wa shirika la ferry wakisema wanatumia mvua kama kisingizio.

Nae Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho ameikashifu serikali kuu akidai kuwa haijatafuta mbinu ya kutatua matatizo ya kila uchao yanayokikumba kivuko hicho.

Joho amesema kwa sasa serikali inafaa kuzingatia kujenga daraja katika kivuko hicho na wala sio kununua au kutengeza Ferry hizo.

 

Show More

Related Articles