HabariPilipili FmPilipili FM News

Baadhi Ya Mitaa Yafurika Mombasa.

Taharuki imetanda katika baadhi ya mitaa hapa Mombasa kutokana na mafuriko yanayoshuhudiwa katika maeneo mengi ya kaunti.

Wakazi wengi katika maeneo hayo wanahofia kuwa huenda baadhi ya nyumba zao zikabomoka kutokana na hali hiyo, huku wengine wakilalamikia kuzorota kwa biasahara zao.

Katika baadhi ya mitaa watu wanalazimika kutoa shilingi hamsini ili kubebwa mgongoni.

Katika kaunti ya kilifi hali sawia na hiyo imeshuhudiwa eneo la Mbogolo pale sehemu ya barabara ilipokatwa na mafuriko na kukatiza usafiri.

Hali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Mombasa kuelekea malindi huku watumizi wa barabara hiyo wakihimizwa kutumia barabara ya Mavueni Kaloleni.

 

Show More

Related Articles