BiasharaPilipili FmPilipili FM News

EPZA Waonyesha Bidhaa Walizotengeneza Mombasa.

Wakaazi wa Mombasa wamemiminika katika ukumbi wa visa oshwal kujinunulia nguo ambazo zimetengenewa na kampuni za epz humu nchini.

Maonyesho hayo ya kuuza bidhaa zilizotengenezwa humu nchini yatadumu kwa siku tatu na katibu katika wizara ya biashara na viwanda nduati mwangi amezipongeza kampuni za EPZA kwa kuamua kuweka maonyesho hayo ili wananchi waweze kununua kwa beo nafuu

Huku akiwahimiza wauzaji wa nguo za mitumba kuwa soko lao halijamalizwa bali wanafaa na kushirikiana na kampuni hizi.

Naye mbunge wa Msambweni Suleiman Dori amesifia hatua hio akisema hali hii inapaswa kuendelea na hata kuandaliwa kila mwezi katika kila mji humu nchini.

Wateja nao hawakuasazwa kwani wamefurahishwa na soko hilo wakisema wamefurahishwa na zoezi hilo ambalo limewafanya kununua bidhaa kwa bei nafuu ikilinganishwa na maduka mengine.

Mzunguko huu wa maonyesho na uuzaji wa nguo zinazotengenezwa humu nchini ulianza jijini Nairobi katika jumba la KICC ambapo rais Uhuru Kenyatta alizindua rasmi na zoezi hili limepangwa kuelekezwa katika sehemu nyengine ya nchi zikiwemo Eldoret,Meru Na Kisumu.

 

 

Show More

Related Articles

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker