HabariMilele FmSwahili

Munyaka: Kila mwanasiasa ana uhuru wa kuamua mwelekeo wake

Wanasiasa wa chama cha Jubilee kutoka Ukambani wamewaonya wenzao wa muungano wa upinzani dhidi ya kuwatenga kwa kutompigia debe kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.Mbunge wa Machakos mjini Victor Munyaka anasema kila mwanasiasa ana uhuru wa kuamua mwelekeo wake wa kisiasa.Anasema japo anaunga mkono kuungana kwa vyama vidogo vya kisiasa kutoka ukambani kuungana kumpigia debe Kalonzo kupeperusha bendera ya muungano wa NASA,watasalia Jubilee na kuelezea imani ya kuhifadhi nyadhfa zao za uongozi.

Show More

Related Articles