HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa wahudumu wa Afya Nandi wanukia

Wahudumu wa afya kaunti ya Nandi wanatisha kugoma katika muda wa wiki mbili zijazo kulalamikia kukawia kwa mishahara yao kwa miezi sita.Mwenyekiti wao Jacob Maswai anasema licha ya kuwasilisha lalama zao mara kadhaa hakuna hatua iliyochukuliwa.Ameitaka serikali ya kaunti kuwapa ajira ya kudumu maafisa 300 anaosema wamefanya kazi kama vibarua kwa muda mrefu.Amelalamikia kutokuweko kwa usawa katika mishahara ya wahudumu wa afya kaunti hiyo na kushinikiza kuainishwa kwa mishahara hiyo mara moja.

Show More

Related Articles