HabariMilele FmSwahili

KNUT yapinga pendekezo la somo la michezo kufanyika wikendi

Chama cha walimu KNUT kimepinga pendekezo la mwajiri wa waalimu TSC kutaka somo la michezo (co curricula activities) kufanywa siku za Jumamosi na Jumapili badala ya katikati ya wiki kama ilivyo kwa sasa. Naibu kaimu mkuu wa KNUT James Ndiku amesema pendekezo hilo linalenga kuhujumu haki za walimu kuabudu au kupumzika. Amesema KNUT inaunga mkono mabadiliko mapya katika sekta ya elimu na kuitaka TSC kuwahusisha wadau wote inapofanya mabadiliko katika sekta hiyo.

Show More

Related Articles