HabariMilele FmSwahili

Rais Magufuli afutilia mbali agizo la kuwalazimu wachumba kuwa na vyeti vya kuzaliwa

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa na waziri wa masuala ya katiba na sheria Harrison Mwakyembe linalowataka watu wanaotaka kufunga ndoa kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia tarehe mosi mwezi Mei 2017.Magufuli amesema serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa,huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.Amesema hadi kufikia sasa idadi ya watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ipo chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi wanaoishi vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

Show More

Related Articles