HabariMilele FmSwahili

Vijana kufaidika na mafunzo ya kimaisha

Zaidi ya vijana 10,500 kutoka kanda ya Kaskazini Mashariki na Pwani wanatarajiwa kufaidi na mpango maalum wa mafunzo kuwawezesha kujiendeleza kimaisha.Mafunzo hayo yatakayofadhiliwa na muungano wa umoja wa Ulaya EU kupitia hazina ya dharura(Emergency Trust Fund) utawafaidi vijana kutoka kaunti za Lamu,Mombasa,Taita Taveta,Tana River,Kwale,Kilifi,Garissa,Wajir na Mandera.Mkuu wa masuala ya uchumi na uongozi katika muungano wa EU Vincent De Boer anasema kati ya vijana hao 6,500 watapokea mafunzo ya kisasa jinsi ya kunufaika na nafasi za ajira huku vijana 4,000 wakipewa mafunzo jinsi ya kukabiliana na majanga na masuala yanayoathiri jamii zao.De Boer anasema lengo kuu la mpango huo ni kukabiliana na ukosefu wa ajira anaosema hauathiri Kenya pekee ila ulimwengu kwa jumla.Mpango huo utaendeshwa kwa kipindi cha miaka minne kwa gharama ya sh.bilioni 1.3

Show More

Related Articles