HabariMilele FmSwahili

NASA yaendeleza kampeni Kajiado

Muungano wa upinzani NASA unapeleka kampeini ya kujipigia debe kaunti ya Kajiado wikendi hii.Vinara watatu wa NASA Kalonzo Musyoka wa Wiper,Musalia Mudavadi wa Amani national congress na Moses Wetang’ula wa Ford-Kenya watakua mjini Kitengela kwa mkutano unaolenga kuwahakikishia wananchi bado wangali pamoja.Kinara mwenza Raila Odinga ambaye hataudhuria mkutano huo yuko nchini Marekani na anatarajiwa kurejea nchini wiki ijayo.mkutano huu unaandaliwa baada ya tetesi kuibuka huenda Kalonzo akajiondoa katika muungano huo wa NASA na kugombea kiti cha urais akiwa huru.Hata hivo Wetangula anasisitiza vinara wote wanne wako pamoja na hawatasambaratika kamwe.

Show More

Related Articles