MichezoPilipili FmPilipili FM News

Michezo Ya Wabunge Yapamba Moto Mombasa.

Michezo ya wabunge wa afrika mashariki inaingia siku yake ya tatu hii leo huku kwenye siku ya pili timu ya soka ya wabunge wa Kenya walianza vibaya michuano hio baada ya kurindimwa bao moja kwa bila na majirani zao kutoka Uganda, wakati huo huo timu ya bunge la afrika mashariki EALA ilianza kutetea taji lao la soka baada ya kudungua Burundi mabao mawili kwa moja  mabao ya EALA yakitiwa kimiani na Jamal Ibrahim huku bao la kufutia machozi na Burundi likifungwa na Cloude.

Kwenye michezo ya netiboli Wabunge wa Uganga walipata ushindi wa bwerere baada ya Wabunge wa Kenya kutotosha uwanjani.

Katika michezo ya voliboli  wanaume nikuwa wabunge wa Uganda waliwatandika wabunge kutoka kwa Magafuli seti mbili kwa bila za( 25,12)  (25,12), timu ya Rwanda ikapata mteremko kwa ushindi wa bwerere hii ni baada ya Bunge la Burundi kukosa kuwasilisha kikosi uwanjani.

Kwenye upande wa voliboli ya wanawake wabunge warembo kutoka Kenya waliwakamua wenzao kutoka kwa Mseveni seti mbili bila jibu za (26,24) (25,18).

Makala hayo ya saba yanaingia siku ya tatu hii leo ambapo katika netiboli waheshimiwa kutoka Tanzania watakabiliana na wenzao kutoka Uganda kwa upande wa wanawake wakati huo huo warembo wa Burundi wakipige dhidi ya Rwanda, kwa upande wa wanaume kitengo cha voliboli Uganda wataonyeshana ubabe na wabunge wa Kenya huku EALA wakabiliane na Burundi.

Katika soka Tanzania watanukishana kikwapa na Uganda huku Burundi wakipige dhidi ya Rwanda.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.