HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Haniyah Sagar akanusha kuhusika na shambulizi la Central

Mjane wa marehemu Aboud Rogo, Haniya Said Sagar amekanusha mashtaka dhidi yake kuhusiana na shambulizi la kigaidi katika kituo cha polisi cha Central jijini Mombasa kilichotokea.
Haniya Sagar ameshtakiwa kwa kosa la kutotoa habari kwa maafisa wa polisi kuhusiana na shambulizi hilo kufuatia madai ya uhusiano wake na washukiwa wakuu kwenye shambulizi hilo..
Mbali na hayo, seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amepewa makataa ya miezi miwili kumfikisha mahakamani mwenyekiti wa kikundi cha MRC Omar Mwamnuadzi anayetafutwa na mahakama, Sonko alikuwa amemsimamia kiongozi huyo kwa kumlipia dhamana mahakamani Mombasa.

Show More

Related Articles