HabariMilele FmSwahili

Maelfu ya lita za pombe haramu zanaswa Eldoret

Mafisa wa polisi mjini Eldoret wamenasa maelfu ya lita za pombe haramu katika maeneo sugu ya kutengenezea pombe huku machifu na manaibu wa machifu wa sehemu hizo wakiachishwa kazi. Kamishna wa kaunti ya uasingishu Abdi Hassan amesema watu wawili wametiwa mbaroni  huku akiahidi kikosi maalumu cha kupambana na pombe hiyo  kitapiga Doria sehemu hizo kila siku. Hassan aidha a mesema magari yanayohusishwa na usafirishaji   pombe   hizo kutoka taifa jirani  yanachunguzwa na huenda leseni yao ikatwaliwa na mamlaka.

Show More

Related Articles