HabariMilele FmSwahili

Samwel Moroto amemsuta Matiangi kwa madai ya usimamizi mbaya ya sekta ya elimu

Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amemsuta waziri wa elimu Fred Matiangi kwa madai ya usimamizi mbaya wa sekta ya elimu. Moroto amemtaka Matiangi kukomesha kile anadai ni udikteta katika sekta hiyo huku akikosoa matamshi yake ya hivi majuzi kuhusiana na viongozi waliokosoa uteuzi wa kaimu naibu chansela wa chuo kikuu cha Moi profesa Laban Ayiro. Akizungumza katika shule ya upili ya Kaibos Moroto hata hivyo amewaonya viongozi dhidi ya kuingiza siasa na ukabila katika maswala ya uongozi wa taasisi za elimu nchini.

Show More

Related Articles