HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Shinyalu awapa majukuma mawili Jackson Mandago na Alex Tologos kujiuzulu

Mbunge wa Shinyalu Silverse Anami lisamula awapa majuma mawili magavana wa kaunti za Uasin Ngishu na Elgeyo Marakwet kujiuzulu kwa kupinga uteuzi wa kaimu naibu chansela wa chuo kikuu cha Moi profesa Laban Ayiro. Anami anasema gavana Jackson Mandago wa Uasin Ngishu na Alex Tolgos wa Elgeyo Marakwet wamedhihirisha ukiukwaji wa kipengee cha katiba kuhusu uongozi na maadili kufuatia hatua yao. Ameitaka tume ya uiano na utamgamano NCIC kuwachukulia hatua za kisheria huku pia akishinikiza kutimuliwa kwao iwapo hatawajiuzulu.ametoa wito kwa rais Kenyatta na naibu wake william Ruto kuangilia swala hilo akisema linatishia kuzua uhasama wa kijamii nchini

Show More

Related Articles