HabariMilele FmSwahili

Kinara wa CORD Raila Odinga amsuta seneta Dan Mwanzo kuwa msaliti

Kinara wa CORD Raila Odinga amemsuta seneta wa Taita Taveta Dan Mwazo na kumtaja kama msaliti kwa kukigura chama cha ODM. Akiongea katika eneo la Kasigau Raila anasisitiza chama cha ODM kiko imara licha ya baadhi ya wanachama kutangaza kujiunga na Jubilee. Hata hivyo Mwazo amesusia ziara ya Raila kaunti hiyo.Raila anatazamiwa kuelekeza ziara yake huko kwale ambako swala la uasi pia litashamiri haswa baada ya gavana Salim Mvurya kutangaza kuhama ODM na kujiunga na Jubilee.

Show More

Related Articles