HabariMilele FmSwahili

Shirika la kutetea haki za binadamu lataka jumuiya ya ulaya kupuuza wito wa nchi za Afrika kumaliza uhusiano na mahakama ya ICC

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch lataka mkutano wa jumuiya ya ulaya na baraza la usalama la umoja wa mataifa utakaofanyika kesho kutupilia mbali wito wa nchi za Afrika kumaliza uhusiano na mahakama ya ICC. Shirika hilo linasema nchi za Afrika zinafaa kushirikiana na ICC ili kuimarisha utendakazi wake badala ya kupanga njama ya kujiondoa. Mwakilishi wa tume ya kimataifa ya wanasheria ICJ Stella Ndirangu anaonya kuwa jaribio la kujiondoa kwa Afrika ni njama ya baadhi ya viongozi kutaka kukwepa kuchukuliwa hatua wanapohusika katika vitendo vya ukiukwaji haki za raia.

Show More

Related Articles