HabariMilele FmSwahili

Gavana Kidero akubali kumlipa Ondiek milioni 8.8 kwa kumuondoa afisini bila kuzingatia sheria

Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero amekubali kumlipa milioni 8.8 aliyekuwa waziri wa mazingira katika bunge la Nairobi Evans Ondiek kwa kumuondoa afisini bila kuzingatia sheria. Katika waraka, Kidero ameridhia agizo lililotolewa na mahakama agosti 22. Ondiek aliwasilisha kesi mahakama akidai Kidero alimfurusha uongozi kwa sababu za kisiasa, madai ambayo Kidero alipinga akidai hatua yake ilinuia kuhakikisha utendakazi bora katika kaunti.

Show More

Related Articles