HabariMilele FmSwahili

Polisi wanazuilia washukiwa 2 watengenezaji wa pesa bandia Kitui

Polisi toka Ikutha kaunti ya Kitui, wanawazuilia washukiwa wawili wa watengenezaji wa pesa bandia baada ya kuwanasa wakiwa na shilingi milioni moja unusu bandia. OCPD wa Ikutha Clifford Nyagah amesema pesa hizo zilipatikana zikiwa zimefichwa ndani ya karatasi katika duka soko eneo hilo. Anasema polisi pia wamepata baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia kutengeneza pesa hizo. Washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Ikutha wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Show More

Related Articles