HabariMilele FmSwahili

Waziri wa elimu kuongoza hafla ya kufuzu kwa wanafunzi katika chuo cha Moi

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi anatarajiwa kuongoza hafla ya kufuzu kwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Moi. Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi kumlaumu kwa kumteua prof Laban Ayiro kama kaimu naibu chansela wa chuo kikuu cha Moi. Viongozi wa eneo hilo wanamshutumu matiangi kwa kumteuwa perofesa Laban Ayiro kwa njia isiyofaa. Issack Melly ni seneta wa uasin ngishu. Aidha seneta Melly ameyataja kama propaganda madai kuwa huenda hafla ya leo ya kufuzu kwa wanafunzi ikatatizwa kulalamikia hatua ya MatiangiWakati huo huo waakilishi wadi kaunti ya Vihiga wametoa wito kwa naibu rais William Ruto Kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro huo. Wamelaani kile wanakitaja kama ubaguzi wa kikabila kuhusiana huku wakisema profesa Laban Ayiro kama mkenya mwengine ana haki ya kufanya kazi popote nchini.

Show More

Related Articles