HabariMilele FmSwahili

Waziri Fred Matiangi apuuza vitisho vya viongozi kutoka Uasin Gishu

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi amewapuzilia mbali viongozi kutoka kaunti ya Uasin Gishu wanaopinga uteuzi wa prof Laban Ayiro kama kaimu naibu chansela wa chuo kikuu cha Moi.Matiangi anasema prof Ayiro ameteuliwa kuambatana na sheria na endapo kuna malalamishi yoyote kuna utaratibu wa kufuatwa.
Amesema haya huku prof Ayiro akichukua rasmi wadhfa huo. Akizungumza baada ya kupokezwa vifaa vya kazi na mtangulizi wake prof Richard Mibey, Ayiro ameomba kupewa fursa ya kuchapa kazi akitaka ushirikiano kutoka wadau wote.

Show More

Related Articles