People Daily

Kiongozi wa waasi nchi ya demokrasia ya Kongo Bosco Ntaganda amaliza mgomo wa kula

Kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Bosco Ntaganda anayezuiliwa korokoroni katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC huko the Hague hatimaye amemaliza mgomo wa kula wa wiki mbili. Ntaganda aligoma kula kulalamikia hali anayopitiia korokorini ikiwemo kutoweza kukutana na jamaa zake. Anakabiliwa na mashitaka 18 yakiwemo ya mauaji, kuwatumia watoto kama wanajeshi na wanawake kama watumwa wa ngono.

Show More

Related Articles