HabariMilele FmSwahili

Wavinya Ndeti awataka wanasiasa kuendesha kampeni za amani

Kiongozi wa chama cha uzalendo CCU Wavinya Ndeti anawataka wanasiasa kuendesha kampeini za amani taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu. Bi.Ndeti anasema wanasiasa wana jukumu la kuhakikisha amani na utulivu unaoshuhudiwa nchini kwa sasa hautatizwi na kampeni zao. Hayo yakijiri,Bi.Ndeti amesema chama cha CCU kitamuunga mkono kiongozi wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka kupeperusha bendera ya CORD katika kinyanganyiro cha urais uchaguzi mkuu ujao.

Show More

Related Articles