HabariMilele FmSwahili

Mhudumu wa boda boda auwawa na umati Kakamega

Mhudumu wa boda boda ameuwawa na umati uliomfumania akisafirisha kondoo wawili wanaodaiwa kuibwa katika eneo la Mautuma huko Lugari kaunti ya Kakamega. Chifu wa sehemu hiyo Peter Lugano anasema mwendazake Bramwel Bakika mwenye umri wa miaka 26 alifumaniwa akiwasafirisha kondoo wawili kwenye pikipiki yake na kuuwawa aliposhindwa kuelezea alikowatoa. Lugano amewaonya wananchi dhidi ya kujichukulia sheria mikononi badala yake kuwakabidhi washukiwa kwa huku akiwataka kuwakabidhi kwa polisi ili hatua ichukuliwe dhidi yao.

Show More

Related Articles