HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Raila azuru kaunti ya Taita Taveta kuendeleza mikakati yake

Chama cha ODM kinapania kuwafurusha viongozi kumi na watatu ambao walichaguliwa chini ya chama hicho, lakini wakakihama na kujiunga na vyama vingine.
Kwenye barua iliyotiwa sahihi na mwenyekiti wa nidhamu ya chama cha chungwa Fred Athuok, viongozi hawa wanaojumuisha magavana, wabunge na hata wawakilishi wa akina mama bungeni wana muda wa siku saba kujitetea mbele ya usimamizi wa chama hicho, la sivyo wafurushwe.
Haya yamesemwa wakati kinara wa chama Raila Odinga amerejea katika maeneo ya Pwani kwa mara ya pili chini ya mwezi mmoja, kukipogia debe chama hicho.

Show More

Related Articles