HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa madaktari wasitishwa katika kaunti ya Nyeri

Madakitari huko Nyeri wamesitisha mgomo wao ulianza ijumaa iliyopita.Madaktari hao wanasema mazungumzo baina yao na uongozi wa kaunti yamezaa matunda matakwa yao yakiangaziwa.Hapa Nairobi madaktari wanaogoma kaunti ya Nairobi wametakiwa kurejea kazini kufikia mwisho wa siku leo au wafutwe kazi.Katibu wa kaunti Robert Ayisi anasema iwapo madaktari hao watakaidi agizo hilo basi nafasi zao zitatangazwa wazi.Anasema mgomo huo ni haramu kwani matakwa ya madaktari hao yameangaziwa.Madaktario wanaogoma wanalalamikia mishahara duni,kupandishwa vyeo na hata mazingira yasioridhisha ya kufanyia kazi.

Show More

Related Articles