HabariMilele FmSwahili

Uganda na Ufaransa zatia saini ya ushirikiano wa kijeshi

Uganda na Ufaransa zimesaini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi kufuatia mkutano wa marais Yoweri Museveni rais Francois Hollande mjini Paris. Ufaransa sasa itasaidia Uganda katika mafunzo mbalimbali ya kijeshi na pia kuwauzia silaha. Rais Hollande ameipongeza Uganda kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuna amani, utulivu na usalama katika eneo la Afrika mashariki.

Show More

Related Articles