HabariMilele FmSwahili

Takriban nusu ya kinamama kaunti ya Lamu hawatumii tembe za kuzuia uja uzito

Takriban nusu ya kinama kaunti ya Lamu hawatumii tembe za kuzuia uja uzito. Baraza la idadi ya watu linasema utafiti umeonyesha asilimia 50 hawana ufahamu na hawatumii tembe hizo. Mwenyekiti wa baraza hilo Simon Pepee anasema hata hivyo asilimia 70 ya wanaumme kaunti hiyo wanatumia mipira ya kondomu.Ameelezea haja ya hamasisho kwa wenyeji kutambua umuhimu wa kutumia mbinu tofauti za uzazi ili kujifungua watoto kulingana na uwezo wa kuwakimu.

Show More

Related Articles