HabariMilele FmSwahili

NTSA yasimamisha kwa muda leseni za mashirika 5 ya magari ya uchukuzi wa umma

Mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA imesimamisha kwa muda leseni za mashirika matano ya magari ya uchukuzi wa umma. Katika taarifa mkurugenzi mkuu Francis Meja anasema magari hayo yameendelea kukiuka sheria za trafiki. Ameiagiza idara ya trafiki kuyakamata magari ya mashirika hayo yatakayoendelea kuhudumu. Magari hayo ni ya Kisumu Ahero Mowouk Sacco,Daima Connection Ltd Sacco,Narok Line Services Sacco,Sema Stage Sacco na Mwingi Travellers Sacco

Show More

Related Articles