HabariMilele FmSwahili

Mutahi Ngunyi arejeshea serikali millioni 11.8

Mchaganuzi wa masuala ya siasa Mutahi Ngunyi ameirejeshea serikali shilingi milioni 11.8 fedha alizolipwa na shirikia la NYS. Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu uhasibu, Ngunyi anasema alirejesha fedha hizo jana kupitia benki kuu baada ya kubaini alilipwa kiwango cha juu zaidi ya kile alistahili kupokea kutokana na kandarasi aliyopokea. Ametetea kampuni yake ya Consulting House akisema iliibua madai kuhusu viwango vya juu vya bajeti vilivyotengewa miradi tofauti ya NYS lakini haikuwa na uwezo wa kutoa taariaf hizo kutokana na mkataba baina yake na NYS amekanusha madai ya mfanyibiashahara Josephine Kabura kuwa alihusika katika kula njama ya kufuja fedha za NYS. Ngunyi ametajwa kwenye sakata ya shilingi milioni 791 fedha za NYS.

Show More

Related Articles