HabariMilele FmSwahili

Hassan Noor Hassan kuhojiwa na tume ya EACC leo

Mshauri mkuu wa maswala ya ugatuzi Hassan Noor Hassan anahojiwa leo katika makao makuu ya tume ya kukabiliana na ufisadi EACC kuhusiana na utoaji zabuni ya huduma za ushauri. Noor ambaye ni mkuu wa zamani wa mkoa wa Rifty Valley ametakiwa kufika mbele ya makachero wa EACC saa tatu unusu asubuhi. Anahitajika kutoa maelezo kuhusiana na madai ya utoaji kinyume cha sheria wa ushauri kwa maafisa wa wizara ya ugatuzi mwaka 2014/15.

Show More

Related Articles