HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi wa kike anauguza majeraha baada ya kudungwa kisu na mwenzake

Mwanafunzi mmoja wa kike katika shule ya upili ya St. Michael anauguza majeraha mabaya baada ya kudungwa kisu na mwenzake. Kwa mujibu wa walioshuhudiwa, wawili hao walionekana wakizozana kabla ya mshukiwa kutekeleza kitendo hicho. Chifu wa Bomet Township Reuben Ngetich anasema mwathiriwa amelazwa nkatika hospitali ya mishonari ya Tenwek akiwa katika hali dhabiti. Mshukiwa aliye katika kidato cha tatu naye anazuiliwa katika kituo cha polisi mjini humo akisubiri kufikishwa mahakamani hapo hii leo.

Show More

Related Articles