HabariMilele FmSwahili

Tanzania yatangaza hatua mpya za kukabili usafirishaji wa binadamu

Serikali ya Tanzania imetangaza hatua mpya za kukabiliana na usafirishaji wa binadamu. Naibu waziri wa mambo ya ndani nchini humo Hamad Yusuf Masauni amesema, nchi hiyo imekuwa chanzo, kituo, na kikomo cha usafirishaji haramu wa binadamu. Amesema hatua hizo zitajumuisha idara zote za usalama na wananchi, zikiwa na lengo la kuwakamata watu wanaofanya biashara hiyo ya kikatili. Pia amesema, maofisa wa uhamiaji ambao maeneo yao yanatumika kama njia ya kupitishia watu watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Show More

Related Articles