HabariMilele FmSwahili

Wenyeji wa Kerio wamtaka Asman Kamama kuwahakikishia usalama wao

Viongozi kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet wametoa makataa ya siku saba  kwa wakuu wa idara ya usalama na mbunge wa eneo la Tiaty Asman Kamama kuwahakikishia usalama wao la sivyo waandae kulalamikia ongezeko la vifo vinavyosababishwa na wizi wa mifugo eneo la bonde la Kerio.Wakiongozwa na Moses Bowen, viongozi hao wanahoji kuwa zaidi ya watu 20 wamepoteza maisha huku mifugo elfu 30 wakibwa kutoka kutokana na utepetevu wa maafisa wa usalama. Wanaitaka serikali kuu kuwapokonya silaha haramu wenyeji katika kaunti hii.

Show More

Related Articles