HabariMilele FmSwahili

Muungano wa wachapishaji vitabu nchini unataka fedha za kununua vitabu kuongezwa

Muungano wa wachapishaji vitabu umetaka wizara ya elimu kuongeza mgao wa fedha zinazotumika kununua vitabu vya burudani kwa wanafunzi ukisema fedha zinazotolewa kwa sasa hazitoshi. Muungano huo unasema ushuru unaotozwa kwa vitabu umepelekea kutumika kwa fedha zinazostahili kugharamia vitabu hivyo. Mweka hazina wake John Mwazemba anasema gharama hizo na ukosefu wa vitabu vya kutosha kunaathiri uwezo wa wanafunzi wa kusoma kwa kukosa mazoezi.Wanasema ni hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu.

Show More

Related Articles