HabariPilipili Fm

Mfumo Mpya Wakusajili Wanafunzi Kutumika TUM.

Chuo cha kiufundi cha TUM hapa Mombasa kinapania kusajili wanafunzi wake wote kupitia mfumo wa kielektroniki wa BVR katika mpango maalum wa kuthibiti misimamo mikali pamoja na shughuli zinazohusiana na ugaidi.

Kaimu naibu chansella wa chuo hicho Laila Abubakar amesema zoezi hilo, linalotarajiwa kung’oa nanga juma hili, limelenga kuboresha mfumo wa kuwatambua wanafunzi wake, na kuwazuia kujificha na makundi ya kigaidi.

Laila ametoa onyokali kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kwa mara ya kwanza mwaka huu wa 2016, akisema chuo cha TUM hakitaruhusu wanafunzi wanaojihusicha na masuala ya itikadi kali na ugaidi.

Kuhusiana ma masuala ya elimu amehimiza wanafunzi kupatia elimu kipaombele, akiongeza kuwa wale ambao hawataafikia matarajio ya chuo hicho huenda wakapewa adhabu kali.

Show More

Related Articles