HabariMilele FmSwahili

Serikali imetetea hatua yake ya kuwataka wanawake wa kiislamu kuvua hijab katika sehemu za umma

Serikali imetetea hatua yake ya kuwataka wanawake wa kiislamu kuvua vazi la hijab wanapooingia sehemu za umma ikisema ni njia moja ya kudumisha usalama. Naibu kamishna kaunti ya Mombasa Mahmoud Salim anasema mpango huo utawasaidia kuwatambua wahalifu. Ametoa mfano wa washukiwa 3 wa ugaidi waliowawa baada ya jaribio la kushambulia katika kituo cha Central huko Mombasa kutibuka nayo jamii ya wasomali ikiongozwa na Abdi Mohammed imelalamikia kuhangishwa kwa waislamu kutokana na vitendo vya watu wachache wanaodaiwa kuwa washukiwa wa ugaidi.

Show More

Related Articles