HabariMilele FmSwahili

Daktari anazuiliwa na polisi kwa kusababisha kifo cha msichana wa miaka 13 Narok

Daktari mmoja anazuiliwa na polisi kwa kusababisha kifo cha msichanawa miaka 13 baada ya kumpa dawa za mifugo ili kuavya mimba eneo la Kuto, Narok Magharibi. Mshukiwa anadaiwa kumpa marehemu dawa hiyo katika duka lake la kuuza dawa za mifugo mjini Mulot muda mfupi kabla ya kifo chake. Jamii ya marehemu inasema haina uwezo wa kufuatilia kesi hiyo na sasa inatoa mwito kwa serikali kuhakikisha haki inatendeka. Chifu Joseph Korir ameeleza kuwa mshukiwa alikamatwa akiwa mafichoni huku akiongeza kuwa ukaguzi umeanzishwa kubaini uhalali wa maeneo yakuuzia dawa eneo hilo.

Show More

Related Articles