HabariK24 TvMichezoSwahiliSwahili Videos

Ernest Ngeno na Sheila Chepkurui ndio washindi wa awamu ya mwaka huu ya mbio za barabarani za Kericho

Ng’eno aliyeshiriki mbio za masafa marefu kule Milan mapema 2016 alitamatisha mbio hizo kwa dakika 26 na sekunde 16 , dakika tatu mbele ya Patrick Kipng’eno huku Dennis Chemkwony akiridhika na nafasi ya tatu.
Katika kitengo cha wanawake , Sheila Chepkurui alimaliza kidedeani kwa dakika 36 na sekunde 16 huku Fancy Chemutai na Sheila Chelangat wakimaliza nafasi ya 2 na 3 mtawalia .
Msururu wa riadha unaodhaminiwa na Safaricom utaelekea kwenye mbio za masafa marefu za Mombasa.

 

Show More

Related Articles