HabariMilele FmSwahili

Raila; Sijutii matamshi yangu kuhusu msimamo wa kisiasa wa mwendazake mzee Ntimama

Kinara wa upinzani Raila Odinga anasema hajutii matamshi yake kuhusu msimamo wa kisiasa na maono wa mwendazake mzee William Ole Ntimama. Raila ambaye yuko ujerumani anasema ntimama alikuwa mstari wa mbele kupigania haki na usawa kwa hivyo ripoti ya TJRC inapaswa kupasishwa kwa haraka. Anasema masuala yalio katika ripoti hiyo pia yanahusu taifa la kenya kwa ujumla kwa kuangazia marekebisho katika sekta ya ardhi, umaskini na ukosefu wa usawa na kulindwa jamii ndogo nchini. Raila anasema kamwe hataomumba msahama rais Uhuru Kenytta ambaye alionekana kukerwa na usemi wake katika hafla hiyo iliyoandaliwa nyumbani kwa mwendazake Ntimama huko Mutonyi kaunti ya Narok.

Show More

Related Articles