HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Mjane wa Aboud Rogo kizimbani

Mahakama ya Mombasa inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusiana na iwapo mjane wa marehemu Shekhe aliyekumbwa na utata Aboud Rogo, Hernia Said Saggar, atazuiliwa kwa siku 14 kama uongozi wa mashtaka unavyotaka.
Uongozi wa mashtaka umetoa ombi la Hernia kuzuiliwa kwa wiki mbili ili kuwapa polisi muda zaidi wa kufanya uchunguzi.
Mwanamke huyo alikamatwa nyumbani kwake eneo la Kanamai kaunti ya Kilifi kwa madai ya kuhusika na uvamizi wa kituo cha polisi cha Central katika kaunti ya Mombasa.

Show More

Related Articles