HabariMilele FmSwahili

Marekani itaunga mkono mpango wa kuiwekea Sudan Kusini vikwazo vya silaha

Balozi wa marekani katika umoja wa mataifa Samantha Power amesema nchi yake itaunga mkono mpango wa kuiwekea vikwazo vya silaha Sudan Kusini ikiwa serikali ya nchi hiyo itaendelea kuwazuia askari wa kulinda amani kuwalinda raia. Viongozi wa Afrika walitoa wito wa kupelekwa kwa askari zaidi baada ya mapigano makali kuzuka katika mji wa Juba mwezi Julai na kurudisha nyuma jitihada za kumaliza vita ambavyo vimelikumba taifa hilo tangu mwezi Disemba mwaka 2013

Show More

Related Articles