HabariMilele FmSwahili

Kundi la vijana wa kiislamu KMYA Mombasa waitaka serikali kuimarisha usalama

Chama cha vijana wa dini ya kiislamu huko kilifi KMYA kinaitaka serikali kuimarisha usalama eneo la Pwani kufuatia kisa cha hivi majuuzi cha jaribio la shambulizi dhidi ya kituo cha polisi mjini Mombasa. Mshirikishi wa chama hicho kaunti ya Kilifi Asili Gandani anasema serikali inapaswa kutia maanamani na kuchukuwa hatua za haraka inapopokea maelezo ya kijasusi kuhusu uvamizi kabla haujatekelezwa. Pia ametaka wakaazi wa Pwani kushirikiana na polisi kupitia kuwafichua washukiwa wa ugaidi baada ya ripoti kuibuka kuwa wanawake watatu waliojaribu kushambulia kituo cha Central Mombasa walikuwa wameteuliwa kujiunga na kundi la kigaidi la ISIS.

Show More

Related Articles