HabariMilele FmSwahili

Waziri wa fedha kaunti ya Uasin Gishu mashakani

Bunge  la kaunti ya  Uasin Gishu limepitisha  pendekezo la kumshurutisha waziri wa fedha   kaunti hiyo kuwasilisha mapendekezo ya  mswada  wa  fedha  ambao  una siku kumi na saba kupitishwa kwa mujibu wa sheria.Wawakilishi wadi wakiongozwa na  Jeremiah Sang  wamesema sharti wananchi wapewe muda  kutoa  mchango wao.  Hii ni baada ya mkaguzi mkuu wa umma kukatalia mapendekezo  ya mswada huo   baada  ya  waziri wa fedha  kushindwa kuelezea sababu za  kutenga  zaidi ya millioini 40 kwa matumizi ya afisi  ya gavana.

Show More

Related Articles